Kalenda ya uzazi wa mpango ni mojawapo ya njia za asili zinazotumiwa na wanawake wengi kudhibiti uzazi bila kutumia dawa au vifaa vya kisasa. Njia hii hufanya kazi kwa kuzingatia mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kutambua siku ambazo yai hutolewa (ovulation).
Changamoto kubwa ni kwamba wanawake wengi hutumia kalenda bila kuelewa kanuni za msingi za mahesabu ya siku za hatari. Wengine huhesabu kuanzia siku ya mwisho ya hedhi badala ya siku ya kwanza, au hutumia mzunguko usio sahihi. Makosa haya husababisha kushindwa kwa njia hii.
Kalenda hufaa zaidi kwa mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi ulio sawa kila mwezi. Ili iwe salama, ni muhimu kufuatilia mzunguko kwa miezi kadhaa na kuhesabu siku za hatari kwa usahihi. Elimu sahihi ndiyo nguzo ya mafanikio ya njia hii.